Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga ameshiriki katika kilele cha siku ya Sheria nchini (Law Day) sherehe hizo hufanyika 01 ya mwezi Februari kila mwaka.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Mahakama Wilaya ya Liwale na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara mbalimbali Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wananchi na Watuishi wa Mahakama.
Sherehe hizi zilitanguliwa na wiki ya Sheria nchini iliyo anza kuazimishwa kuanzia january 24 hadi 30 2024 kwa kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi wa Wilaya ya Liwale na viunga vyake ambapo watu mbalimbali waliweza kufikiwa na kuhudumiwa wiki ya Sheria mwaka 2024 imeadhimishwa ikisindikizwa na kauli mbiu isemayo “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa Nafasi ya Mahakama na Wadau Katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai”.
Katika kuadhimisha kilele cha siku ya sheria nchini Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga ameiyomba Mahaka kuhakikisha inatoa haki na kwa haraka kusiwepo na sababu ya kesi kucheleweshwa Mahakamani kwani kesi nyingi zimekuwa zikichukua mda mrefu hivyo kufanya wananchi kupoteza imani na Mahakama zetu.
Mheshimiwa Mlinga ameiyomba Mahakama pia kuhakisha inasaidia kutoa elimu hususa kwa wafugaji na wakulima kuko kumekuwa na migogoro husasa kipindi hiki cha kilimo hivyo Mahakama isaidie kutoa elimu watu waweze kuelewa na pia upande wa mirathi Mahakama itusaidie kuelimisha jamii ili kuondoa mgogoro tumeona familia nyingi zinapoteza mwelekeo kwa sababu ya mirathi hivyo Mahakama mtusaidie ili jamii iweze kuelewa.
Pia Mheshimiwa Mlinga amewataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na Mahakama kwani mahakama ni chombo muhimu sana na ndio kinachotoa haki hivyo pale tunapokuwa na matatizio ya kisheria tuweze kufika mahakamani na tupewe huduma pamoja na haki pia.
Picha mbalimbali katika siku ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo imefanyika katika Mahakama ya Wilaya ya Liwale na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo Vyombo vya ulinzi na usalama wilaya, watumishi wa mahakama, wakuu wa idara mbalimbali, wananchi pamoja na wadau wa sheria.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.