Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amezindua kituo cha afya cha Ngongowele ambao ujenzi wake umegharimu jumla ya shilingi milioni 263,700,000 ambayo fedha kutoka Serikali kuu ni jumla ya 250,000,000 na shilingi milioni 13,700,000 ni kutoka katika Serikali za vijiji vya Ngongowele, Ngunja, na Mikuyu.
Kituo cha afya cha Ngongowele kimekamilisha majengo mawili ya OPD na Maabara ambayo itasaidia kuimarisha huduma za afya lakini pia itaunganisha vijiji na Kata jirani kama Lilombe, Mpigamiti, kuweza kupata huduma katika kituo hicho cha Afya cha Ngongowele
Mheshimiwa Mlinga mewasisitiza wananchi pamoja na watumishi kuhakikisha wanalinda majengo na kutunza vifaa tiba ili wananchi waweze kupata huduma bora na pia amewataka wananchi kuwatunza watumishi wa afya kwani kufanya hivyo kutawafanya wasihame katika vituo vyao vya kazi
Pia amewataka wananchi wa Kata ya Ngongowele kuhakikisha wanachangia pindi wanapopata huduma katika kituo hicho ili kiweze kujiendesha kwa vitu vile vidogovidigo licha ya hilo pia amewakumbusha watumishi kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi, na viongozi wa vijiji na Kata wanao wakuja kupata huduma katika kituo hicho cha afya na pia kituo kitoe huduma kwa Kata zote za jirani bila upendeleo
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewahakikishia wananchi wa Kata ya Ngongowele kuwa Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwahudumia kwa kuwapa vifaa tiba ambapo mpaka sasa Serikali imetoa milioni 200 kwajili ya kununua vifaa na pia kuna miradi mbalimbali inaendelea katika kata hii ya Ngongowele ikiwemo maji, umeme na barabara hivyo tuendelee kuinga mkono serikali yetu kwa huduma inazotupatia.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akifungua Kituo cha Afya cha Ngongowele.
Baadhi ya picha mbalimbali katika matukio ya ufunguzi wa Kituo cha Afya Ngongowele.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.