Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Mheshimiwa Geofrey Pinda amekutana na wakazi wa Kijiji cha Kichonda Wilaya ya Liwale na kuwasikiliza katika kuamua juu ya muwekezaji ndugu Msosa Kasimu Said kupewa hekari 1,000 katika Kijiji hicho ili aweze kufanya shughuli za uwekezaji katika kilimo cha alizeti na kuzalisha mbengu za zao la alizeti.
Mheshimiwa Pinda ameanza kwakufanya kikao cha ndani na Viongozi wa kijiji cha Kichonda ili kutambua uhalali na kupitia mikataba ambayo wameingia baina ya mwekezaji na kijiji na kupitia na kujiridhisha na pia kuwasikiliza wanakijiji maoni yao juu ya mwekezaji huyo katika Kijiji cha Kichonda.
Aidha Muheshimiwa Pinda aliwakumbusha wanakijiji wa Kichonda pamoja na muwekezaji juu ya kufuata na kutekeleza yale yaliyo katika mkataba katika kusaidia jamii ikiwemo kuchimba visima viwili vya maji, kujenga ghala la kijiji la kuhifadhi mazao, kujenga wodi ya kina mama hivyo kuhakikisha hayo yote yanatekelezwa kama yalivyo hainishwa napia Waziri Pinda amemtaka muwekezaji kufuata makubaliano na kuomba maamuzi kwa wanakijiji ili mwekezaji apate ardhi.
Pia Mheshimiwa Pinda amesimamia zoezi la upigaji kura ya wazi juu ya wanakijiji cha Kichonda kumkubali muwekezaji apewe ardhi ili aendelee na shughuli za uwekezaji katika kijiji hicho. Hata hivyo baada ya wananchi wa kijiji cha kichonda kupiga kura ya wazi Mheshimiwa Pinda amesema kuwa “baada ya zoezi hili la wanakijiji kupiga kura kukamilika basi taratibu nyingine zitaendelea katika ngazi mbalimbali mpaka kufikia ngazi ya Wizara ili kukamilisha taratibu hizo ili mwekezaji aweze kupata eneo la uwekezaji”.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Pinda amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kuhakikisha anakutana na Waheshimiwa Madiwani katika baraza la dharula ili kuhakikisha na wao wanangalia kama muwekezaji anafaa na kukidhi vigezo ili kuweza kuendelea na taratbu nyingine katika kukamilisha zoezi hilo.
Pia Mheshimiwa Pinda amemtaka muwekezaji kuhakikisha kuwa kuyatimiza yale yote waliyo kubaliana na yaliyopo kwenye mkataba na pia ikiwemo la ushirikiano baina ya muwekezaji na Chuo cha Kilimo cha Sokoine SUA ili taribu nyingine ziendeelee.
baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kichonda wakimsikiliza Naibu waziri wa Ardhi Mheshimiwa Geofrey Pinda katika mkutano ili kumpitisha muwekezaji.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.