Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amekutana na wafanyabiashara wa mazao ya misitu akiwataka wafanyabishara kufuata sheria na kanuni katika uvunaji na pia kulipa tozo zote ambazo zinatokana na mazao hayo ya misitu hayo yamejiri katika kikao ambacho kimefanyika leo kati ya wafanyabiashara hao pamoja na Mkuu wa Wilaya.
Katika kikao hicho Mheshimiwa Mlinga amewambia wafanyabiashara wa mazao ya misitu kuwa misitu ni mingi ndani ya Wilaya ya Liwale ila mapato ni madogo ambayo ayaendani na misitu inayovunwa ndani ya Wilaya hii hivyo ni kwamba wafanyabiashara wengi amlipi tozo za mazao ya misitu kwenye taasisi husika hivyo amewataka wale wote ambao awajalipa tozo zote na leseni zao walipie mara moja kwani mapato hayo ndio yanasaidia kuleta maendeleo.
Mheshimiwa Mlinga pia amewataka wale wote ambao wanatumia leseni za uvunaji ambazo sio zao wakate leseni zao mara moja kwani hawa wamekuwa ndio wakichangia kupotea kwa mapato kutoka na kutofuata utaratibu na hawa amekuwa pia wakizirubuni kamati za maliasili za vijiji kukiuka utarabu ambao upo hivyo kusababisha upotevu wa mapato hivyo ili kuendele na uvunaji kila mmoja awe na leseni yake mwenyewe leseni moja haiwezi ikatumiwa na zaidi ya mtu mmoja.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewataka wavunaji wote kuvuna kwenye eneo ambalo amepewa na sio kuongeaza eneo kwa kuwarubuni kamati za maliasili za vijiji kwani asilimia kubwa hawana uwelewa hivyo wafanyabiashara wanatumia mwanya huo ili kupata sehemu kubwa ya kuvuna kinyume na utaratibu, pia amewataka wale wote ambao leseni zao zinasoma majina yao na awajalipia hivyo walipe pesa zote ambazo wanadaiwa ili kuendelea na uvunaji.
Kwa upande mwingine pia Mheshimiwa mlinga amewataka wavunaji ya misitu kuhakikisha wanafuta taratibu ambazo zipo ikiwemo za wakala wa misitu Tanzania TFS pamoja na zile za Halmashauri na pia kuacha kuchana magogo ambayo ayajagongwa kwani kufanya hivyo ni kuhiujumu Serikali katika kukusanya mapato pia Mheshimiwa Mlinga amepiga marufuku kwa wavunaji wote na wamiliki wa viwanda kuacha kusafirisha magogo na kuchana nyakati za usiku inahatarisha usalama wa raia na pia wavunaji wanasafirisha magogo ambayo ayajakaguliwa na kugongwa.
Baada ya kuzungamza hayo Mheshimiwa Mlinga amebaini kuwa viwanda vingi vinaingiza magogo ambayo ayajagongwa na kukaguliwa na mamlaka husika hivyo wafanyabiashara wakwepa kulipa ushuru “ukizunguka katika viwanda vingi utakuta magogo ambayo ayajakaguliwa na pia ambayo yanasfirishwa usiku mengi yapo hivyo na mengi tumeyakamata katika viwanda hivyo tunawashihi wafanya biashara fateni utaratibu na sheria”.
Pia kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo amewataka wavunaji kuvuna kutokana na leseni yako inavyosema sio vyema kwenda kinyume na leseni ukifanya hivyo ni kosa na pia ni kuipotezea Serikali mapato, pia amewataka kuendelea kutumia mifumo ya ulipaji ambayo ipo kwani Serikali inafanyia kazi na kuendelea kuboresha mifumo ila tufute sheria zinavyo sema.
Mkuu wa wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akizungumza na wavunaji wa mazao ya misitu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.