Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo amefanya kikao na watumishi wote lengo likiwa ni kusikiliza changamoto zao na kuzitatua ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuleta tija kwa Serikali na kuongeza chachu ya kuwahudumia wananchi.
Mkurugenzi amewataka watumishi kuwa na upendo kaitka maeneo ya kazi kwani kupendana kwa watumishi kunasaidia kuongeza ufanisi na utendaji wakazi utaimarika na hata pia fitna hazitakuwepo na hivyo kazi zitafanyika kwa weledi na ufanisi mkubwa., pia ameongeza watumishi kuwa wabunifu katika idara zao na maeneo yao ya kazi na badala yake waondoe dhana ya kuwa walalamikaji “ tukiwa wabunifu kila mtu atatimiza majukumu yake kwa wakati na matokeo yataonekana hivyo tuache kulalamika bali tuwe watendaji”.
Hata hivyo Mkurugenzi amewataka watumishi wote wa umma kuhakikisha wanaisaidia Serikali na kufanya kazi kwa bidii ili iweze kufikia wananchi wote kwakutoa huduma bora kwa wannchi kwa kutimiza majukumu ambayo wamepewa katika idara zote ambazo zipo hapa kwenye Halmashauri lengo ni kutimiza wajibu wako ili wannchi wapate huduma bora.
Aidha Mkurugenzi amewataka watumishi kuwa wadilifu katika kazi zao na kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya simu pindi wanapokuwepo kwenye ofisi za umma na badala yake watumishi wajikite katika kutoa huduma na kusikiliza wananchi na kuwa wabunifu katika idara zao.
Kwa upande mwingine nae Afisa utumishi ndugu Kalokola Kasimbazi amewahasa watumishi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma, na kuwa waadilifu kwa kutii Mamlaka na kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuwahi kazini mapema, kuvaa mavazi ambayo yanaendana na mtumishi wa umma pia kudhibiti matumizi ya ulevi pamoja na madawa ya kulevya katika maeneo ya kazi
Pia awewataka watumishi kuacha kutoa siri na nyaraka za Serikali kwani kufanya hivyo ni kosa napia nikugombanisha kati ya Serikali pamoja na wannchi hivyo sio kitu kizuri na atakaye bainika basi atachukuliwa hatua za kiutumishi pia amewakumbusha kujiepusha na masuala ya kupokea au kutoa rushwa ni kosa kisheria hivyo kila mtu akitimiza wajibu wake basi tutaisaidia Serikali na pia tutaweza kutoa huduma bora kwa wannchi wetu na jamii yetu.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale wakifatilia kwa karibu maagizo ya Mkurugenzi katika kikao cha kazi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.