MKUTANO WA BARA LA MADIWANI
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Liwale, mhe.Mohamed Mtesa ameliomba baraza la madiwani kujadili kwa kina na kuzipatia majibu zile zote changamoto zinazowasilishwa kwenye baraza hilo la robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo leo Madiwani waliwasilisha taarifa zao za kata.Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Liwale,mhe.Mtesa wakati akifungua kikao Cha baraza la madiwani ambapo ameeleza kuwa watumishi wanatakiwa kuhakikisha mapato yanakusanywa vizuri ili kufikia lengo.Aidha mhe.Mtesa amewataka madiwani kujadili kwa kina na kuchukua hatua juu ya suala la wanyama waharibifu linaloikabili halmashauri pamoja na suala la changamoto za wafugaji ambao wapo maeneo ambayo siyo tengefu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.