Mkuu wa wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amefanya ziara wiki hii katika Kata ya Liwale B amabapo amekagua miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara katika vijiji vya Mikunya, Legeza mwendo, na Tuungane ili kusikiliza kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi wa Kata hiyo.
Mheshimiwa Mlinga amewataka wananchi kuwa na ushirikiano na Serikali kwani kero zote amezichukua na atazifanyia kazi na pia waendelee kuwa na imani juu ya Serikali yao inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani imekuwa sikivu na inafanya kazi kwa vitendo.
Akijibu kero za wananchi Mheshimiwa Mlinga amesekuwa suala la wanyama waharibifu tembo Serikali imeendelea kupambana nalo kwa nguvu zote ikiwemo kutumia askari wa wanyama pori na taasisi nyingine ili kudhibit tembo licha ya hilo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani imeleta mradi mpya wa giz ambao utasaidia kutoa mafunzo ya jinsi kupambana na wanyama hao kwa kutoa mafunzo kwa vijana ambao watachukuliwa na kwenda kufundishwa pamoja nakutoa vifaa ambavyo vitasaidia kupambana na tembo sambamba na hilo pia amewakumbusha ahadi ya Mheshimiwa Rais juu ya kulichukua jambo hilo katika ngazi ya kitaifa hivyo tuendelee kusubiri mkakati huo.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewataka viongozi wote wa Vijiji na Kata kuwa na daftari litakalo kuwan a rekodi za waathirika wa wanyama kwani wananchi wengi wamekuwa awaelewi taarifa zao zinpotelewa wapi hivyo ni lazima kuwe na daftari litakalo chukua taarifa zote za msingi za mlalamikaji.
Aidha kutakuwa na mradi wa nyuki ambao utatambulishwa hivi karibuni ambao utatusaidia kupambana na tembo napia utatuongezea kipato kutokana na kuuza asali itakayo zalishwa katika mradi huo ambao unaenda kuanza hivi karibuni.
Pia Mheshimiwa Mlinga amewataka viongozi wote wa vyama vya ushirika kuhakikisha wanawalipa wakulima wote pesa zao na kuacha kusababisha hasara kwa wakulima na ambao wanaendelea na mchezo huo basi Mkuu wa Wilaya amesema atawashughulikia kwani hayupo tiyari kuona wakulima wanachezewa sambamba na hilo nikuhakikisha kila mkulima anapata pembejeo bure kama Serikali inavyotoa hivyo mwananchi atakaye tozwa atoe taarifa.
Kwa upande wa mifugo Mheshimiwa Mlinga amemshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Mohamed Mtesa pamoja na Baraza lake la Madwani kwa kupitisha sheria ya kudhibiti mifugo katika Wilaya ya Liwale hivyo amewakumbusha wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanazitumia sheria hizo pindi wafugaji wanapovamia mashamba hayo au maeneo ambayo siyo kwajili ya ufugaji.
Pia Mheshimiwa Mlinga amemtaka meneja wa Ruwasa Wilaya ya Liwale kuhakikisha mkandarasi anapatikana haraka sana ili afanye kazi kwa haraka ili wananchi wa Kata hii ya Liwale B na vijiji vyake wapate maji safi na salama kwani tiyari Serikali ishatoa pesa.
Mkuu wa Wilaya Goodluck Mlinga pia amewashukuru wananchi wa Kata ya Liwale B kwa kujitokeza kwa wingi katika ziara ya Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Liwale wiki mbili zilizopita kwani kufanya hivyo kuomeonesha ni jinsi gani tunampenda Rais wetu.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Liwale B wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodlack Mlinga katia ziara ya Kata hiyo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.