Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga ametembelea na kukagua mradi wa maji wa Hangai unao lenga kutoa huduma katika vijiji vya Ngongowele, Mikuyu, na Ngunja mradi huo ni muendelezo wa wa utekelezaji wa program ya PforR ambapo jumla ya shilingi 1,318,246,059.65 zimetengwa kutekeleza mradi huo.
Mkataba wa mradi huu ulisainiwa tarehe 06/07/2023 na mkandarasi M/S ULM INVESTIMENT COMPANY LTD kwa gharama ya shilingi 958,975,215.00 ambapo kazi ya kusambaza bomba itafanywa na kiwanda cha Plasco Limited kwa gharama ya shilingi 359, 270,844.65 ambapo mradi unatarajiwa kukamilika tarehe 17/ 04/2024 mpaka sasa jumla ya shilingi 95,897,521.50 zimelipwa kama malipo ya awali.
Mheshimiwa Mlinga amemtaka mkandarasi M/S ULM INVESTIMENT COMPANY LTD wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha kwa wakati ili wananchi wa kata ya Ngongowele na vijiji vyake pamoja na kituo cha afya na shule zinapata maji kwa haraka na pia kuhakikisha vibarua wanao ajiriwa katika mradi huo basi kipaumbele wawe wanatoka Kata ya Ngongowele
Pia Mheshimiwa Mlinga amewataka viongozi na wananchi wa Ngongowele kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili viwezekusaidia maji kupatikana kwa uwakiki na kwa wakati wote hivyo kama kuna mtu atafanya shughuli za kibinadamu katika vyazo vya maji basi ashitakiwe na sheria pia ichukue mkondo wake na pia wafugaji ambao watapeleka mifugo yao kwenye vyanzo vya maji wakamatwe na washitakiwe kutokana na sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akikagua ujenzi wa mradi wa maji Hangai ambao unakwenda kuwasaidia wananchi wa Kata ya Ngongowele na vijiji vyake.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.