Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amefanya mkutano na wahandishi wa habari ikiwa ni kuelezea kazi ambazo zimefanyika na Serikali ya awamu ya sita kwenye mkoa wa Lindi mkutano huo umefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambao humehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa Zainab Talack, Katibu Tawa wa Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa wa Lindi pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi za Serikali.
Katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Talack amesemakuwa Serikali imetoa zaidi ya Trioni moja katika miradi ya maendeleo kwa Mkoa wa Lindi kwa miaka mitatu 2021 mpka 2023 ikiwemo ya Afya, Elimu, Ujenzi wa Mindombinu, ya Barabara, Maji, Kilimo, Umeme na Sekta ya Mifugo.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Talack amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi balimbali katika Mkoa huu jambo linapelekea shughuli za uchumi kuimarika.
Aidha kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo akiwasilisha taarifa yake ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale amesma kuwa katika hawamu ya sita Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi 33, 535,771,764.67 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya, Kilimo, Mifugo, Elimu, na Uwezeshwaji kiuchumi.
Aidha Serikali imewasikia na kuwafikia wananchi Serikali ya awamu ya sita imeiwezesha Halmashauri ya wilaya ya Liwale kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo yenye tija kubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na.
Ujenzi wa ofisi mpya ya Halmashauri kwa gharama ya shilingi 3,000,000,000.00 za ruzuku Serikali Kuu.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kilomita 1.2 wenye jumla ya shilingi 886,659,200 kutoka serikali Kuu.
Ujenzi wa shule za sekondari 2 za Kata ya Kichonda na Mangirikiti na nyumba ya walimu shule ya sekondari ya Mangirikiti wenye jumla ya shilingi 1,135,552,827 za mradi wa SEQUIP.
Ujenzi wa shule mpya ya msingi katika kijiji cha Mbonde wenye gharama ya shilingi 331,600,000.00 kupitia fedha za BOOSTUendelezaji wa ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya kwa fedha za Ruzuku ya Serikali Kuu kwa gharama ya shilingi 3,230,800,000 za Ruzuku Serikali Kuu.
Pia Halmashauri imeendelea kutekeleza miradi midogodogo katika sekta mbali mbali inayohusu ujenzi wa miundombinu muhimu ya kutolea hudumaza kijamii ikihusisha.
Ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari, Ujenzi wa matundu 103 ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari, Ujenzi wa bweni 1 wa watoto wenye mahitaji maalum kwa shule za msingi, Ujenzi wa zahanati 6 mpya, Ujenzi wa nyumba 4 za mtumishi katika zahanati mpya, Ujenzi wa vituo 4 vipya vya afya.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha ambazo ametoa na anendelea kutoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma za kijamii na hivyo kiukweli wananchi wanafurahi sana.
Aidha Msemaji Mkuu wa Serikali amewataka Wakurugenzi wote kuhakikisha wanawatumia vizuri maafisa habari ambao wapo katika Halmashauri zao ili kuweza kutangaza kazi ambazo zimefanyika na pia wananchi wa maeneo hayo wanawajibu wa kujua serikali yao inafanya nini kwenye maeneo yao hivyo tumsaidie Mheshimiwa Rais kuhakisha kazi zinazofanywa na Serikali zinatangazwa.
picha mbalimbali katika mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali katika kuwasilisha kazi za serikali ambazo zimefanyika katika mkoa wa Lindi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.