Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale Ndugu Azilongwa Mwinyimvua Bohari amezindua majengo ya hospitali ya Wilaya ya Liwale ambayo yamekarabatiwa na Shirika la Madaktari wasio kuwa na Mipaka (MSF) ambapo jumla ya kiasi cha shilingi milioni 149,935,995 zimetumika kukarabati jengo la mama na mtoto, jengo la upasaji wodi ya wazazi pamoja na kichomea taka.
Katibu Tawala Bi Bohari amemshukukuru Mkurugenzi wa Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka kwa ukarabati ambao wameufanya katika hospitali ya Wilaya ya Liwale katika majengo haya kwani ni kazi kubwa imefanyika majengo haya yatasaidia kutoa huduma bora za afya kwa mama wajawazito na watoto wachanga.
Aidha Bi Bohari ameliomba Shirika hilo kupitia kwa Mkurugenzi wake Stephani Cornish kuongeza mkataba ili waendelee kutoa huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Liwale hususa wakina mama na watoto kwa sababu hawa ndio wanufaika wakubwa wa huduma hii na pia Wilaya yetu ni kubwa na ina vijiji vingi tunawapongeza kwa sababu mmeweza kuwafika mpaka watu wa vijijini na kuwapa huduma na pia Serikali itaendelea kushirikiana na nyie kwa kila hatua hivyo tunawapongeza kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya kwani mmeweza kutusaidia kutoa madawa, watumishi na huduma nyingine muhimu hivyo tunawashukuru sana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Bwana Stephan Cornish amesama kuwa Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka waliona inafaa kuichagua Wilaya ya Liwale kutokana na changamoto ya watoto wengi na wamama wajawazito kupoteza maisha hivyo wakaona ni vyema kuileta huduma hii katika Wilaya ya Liwale ili kuweza kupunguza na kumaliza kabisa changamoto hii.
“Na leo hii tumejionea wenyewe ukarabati mkubwa ambao umefanywa na shirika hili tumejionea hodi bora kabisa. Majengo mapya kabisa na vifaa vyake ikiwemo jengo la upausuaji pamoja na wodi na lengo letu ni kuhakikisha tunarejesha tabasamu kwa mama wajawazito na watoto wajifungue salama na kupata huduma bora na kufurahi” hata hivyo tunawajibu wakuendelea kufanya kazi na kutoa huduma katika hospitali na vituo vyote vya afya ili watoto na mama wajawazito wafurahie huduma na pia tunaishukurua Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kushirikiana na sisi kwa ukaribu zaidi.
Aidha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Heri kagya amewashukuru wadau hawa madaktari wasiokuwa na mipaka kwa kuendelea kusaidia kutoa huduma hizi za afya hususa kwa mama wajawazito na watoto kwani huduma ambazo zinatoewa ni za ubora kabisa wadau hawa wanatusaidia katika kutoa huduma, kuongeza idadi ya watumishi kwa kuwaajiri na kutoa dawa ambazo zina wasaidia watu wetu hawa hususa hapa Liwale.
Hata hivyo Serikali ipo tayari kushirikiana na nyie wadau wetu na pia tunatamani kuona mnaongeza miradi mingine katika maeneo yetu mengine ya Mkoa wa Lindi ili kuongeza wigo wa utoawaji wa huduma hususa kwa mama wajawazito na watoto wa changa na pia tumeona mchango wenu mkubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora umekuwa mstari wa mbele katika kutoa chanjo mbalimbali kwa watoto wadogo dhidi ya magonjwa ya mlipuko na kutusaidia katika tafiti mbalimbali tunaomba tundelee kushirikiana na Serikali iko tayari kushirikiana na nyie kwa ukaribu .
Kwa upande mwingine Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Liwale Dactari Khadija Kitiku amewashukuru wadau hawa wa madactari wasio kuwa na mipaka kwa msaada wao ambao wanautoa kwa kuwapa huduma bora mama wajawazito na waatoto hususa kwenye vituo vya afya vya vijijini ikiwemo Kimambi, Kibutuka, Lilombe ambavyo vipo mbali na hospitali tunawashukuru kwa msaada wao huu na pia niwaombe wasiishie hapo tu pia tunaomba watusaidie kuatatua changamoto nyingi ambazo bado tunazo hapa ikiwemo kuongeza watumishi wa afya hususa katika hospitali ya wilaya mpya, jenereta la uwakika ili kuweza kutoa huduma bora ambazo tumezikusudaia kuwapa na pia kupunguza na kumaliza kabisa vifo vitokanavyo na uzazi hasa mama wajawazito na watoto hapa Liwale.
Baadhi ya picha Mbalimbali katika uzinduzi wa Majengo yaliyo karabatiwa na MSF shirika la madaktari wasio na mipaka na vifaa tiba mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.