Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amepokea msaada wa mashuka 114 kutoka Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF ikiwa ni kuboresha huduma za kimatibabu ambazo zinatolewea katika hospitali ya Wilaya ya Liwale na vituo vya Afya.
Mheshimiwa Mlinga amewapongeza na kuwashukuru mfuko wa bima ya taifa ya afya kwa kuendelea kutoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya kwani imeongeza hari kwa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na pia kupunguza uhaba wa vifaa ikiwemo mashuka hata hivyo haya mashuka pia yaenda kusaidia vituo vyetu vya afya.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa changamoto ni kubwa kutukona wagonjwa kuwa wengi na pia vituo vya afya ni vingi ndani ya Wilaya ya Liwale hivyo vifaa tiba pamoja na mashuka yamekuwa hayatoshelezi hivyo natoa wito kwa wadau wengine pia waje watusaidie ili tuweze kutoa huduma bora kwa wananchi wetu wa Liwale na pia ameutaka mfuko wa bima ya afya kuendelea kutoa misaada bila kuchoka.
Hata hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Liwale Dactari Benedict John Itu ameshukuru Mkuu wa Wilaya na kwa jitihada zake ambazo anazifanya ili kuhakikisha hospitali ya Liwale inapata vifaa tiba na pia kutafuta wadau muhimu kama hawa ambao wametupa msaada wa mashuka haya ambayo yataenda kupunguza changamoto katika hospitali yetu pamoja na vituo vya afya ikiwemo kwenye wodi za wazazi na watoto pamoja na mama wajawazito.
Hata hivyo “napenda kuwapongeza na kuwashukuru mfuko wa bima ya taifa ya afya NHIF kwa kutukumbuka Liwale na kutuletea mashuka haya yatatusaidia kupunguza changamoto tulizo nazo katika hospitali zetu na vituo vya afaya hivyo hata wagonjwa wakija tutwahudumia vizuri zaidi sababu vitendea kazi vipo”.
Kwa upande mwingine Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF amesama kuwa katika kuunga mkono jitahada za maendeleo za Wilaya ya Liwale ni jukumu la mfuko huo kusaidia jamii kama vile kutoa vifaa tiba pia mfuko wa wa bima ya afya unahudumia watanzania ambao ni wanachama ambao wapo kwenye secta rasmi na mbazo sio rasmi hivyo ametoa wito kuhakikisha watanzia wanajiunga na mfuko huo ili kuhakikisha wanapata matibabu kwa urahisi na kwa gharama nafuu na pia amepongeza jitihada za Mkuu wa Wilaya kwakuhakikisha mashuka haya yanapatikana kwaa jili ya hospitali ya Wilaya na vituo vya afya.
Picha mbalimbali katika zoezi la Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akipokea Msaada wa mashuka toka Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.