TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imefanya zoezi la kugawa ruzuku kwa walengwa wa kaya maskini kwa vijiji vyote ikiwa ni dirisha la mwezi November na Desember na kuwapa elimu mbalimbali ambazo zitasaidia kujikwamua kiuchumi.
Walengwa wamefundishwa jinsi ya kuzuia ukatili wa kijinsia na kuwahabarisha walengwa kuripoti na kuzuia masuala ya ukatili wa kijinsia hata hivyo wameelezwa jinsia inachangia kuwepo na usawa kati ya mwanaume na mwanamke katika mgawanyo wa majukumu ya kijamii, kiuchumi, na kiutamaduni.
Kutokuwepo na usawa baina ya wanawake na wanaume huzuia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii ni vigumu kuondoa umaskini bila kuanzisha mahusiano sawa baina ya wanawake na wanaume, pia walengwa wamefundishwa aina ya ukatili ikiwemo ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono, ukatili wa kisaikolojia, ukatili wa kiuchumi na ukatili wa kiafya pia TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imeendesha zoezi la kuchagua watu mahususi watakao shughulika na masuala ya ukatili wa kijinsia na majukumu yao.
Aidha walengwa wote ambao wanapokea fedha za ruzuku wamehamasishwa kuingia na kutumia katika malipo ya kimtandao ikiwemo kutumia mabenki pamoja na mitandao ya simu ili kuweza kurahisisha malipo kwa walengwa hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imefikia asilimia 47% za walengwa ambao wanatumia mitandao ya simu na mabenki kupokelea fedha zao na lengo likiwa ni asilimia 50% ifikapo mwakani.
Hata hivyo Afisa ufatiliaji TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bwana Prosper Malebo amewataka walengwa ambao wanapokea ruzuku kwaajili ya kunusru kaya maskini kuhakikisha walengwa wanajikita katika uzalishaji ikiwemo kufuga, kuanzisha vikundi kwa ajili ya kukopeshana na pia kuhimizana watu kufanya kazi na kuweka akiba ili kuweza kupunguza umaskini.
Badhi ya walengwa wa ruzuku ya kunusuru kaya maskini wakipokea fedha na kupewa elimu mbalimbali ili kuweza kujikwamua na umaskini.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.