TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imepokea fedha jumla ya shilingi 111,782,705 kwa ajili ya kuwagawia walengwa wa kaya maskini katika vijiji mbalilmbi ndani ya Wilaya ya Liwale kwa wale ambao wametimiza masharti.
Jumla ya idadi ya walengwa wanao lipwa fedha taslimu ni 1,956 na walengwa 1,443 wamelipwa kiasi cha shilingi 94,039,745 moja kwa moja katika akaunti zao za benki pamoja na mitandao ya simu fedha hizi zinajumuisha malipo ya mwezi Jully mpka August 2023 na mwezi september hadi october 2023.
Aidha mratibu wa Tasaf Wilaya ya Liwale Bibi Lucy Kapinga ametoa msisitizo mkubwa na kuwataka walengwa wote ambao wamepokea fedha kuhakikisha wana tumia fedha kwa manufaa ya familia na pia ukiwemo maandalizi ya vifaa vya shule kama sare za shule na kununua pembejeo za kilimo.
Hata hivyo amewataka walengwa kuhakikisha wanakuja kupokea fedha zao wao wenyewe kuepuka kupokeleana na pia kutakuwa na marekebisho ya taarifa za walengwa ambao majina yao yamekosewa na umri hivyo watawasilisha taarifa zao kwa wawezeshaji ambao watakuwa katika vijiji vyao ili ziweze kufanyiwa marekebisho na pia amewakumbusha wazazi kuwa fedha ambazo zimetoka sasa ni kwa masharti ya elimu hivyo wazazi wafanye maandalizi kwa ajili ya kuwapeleka watoto shule.
baadhi ya wanufaika wa Tasaf wakipewa mafunzo na wawezeshaji
picha mbalimbali katika tukio la ugawaji wa fedha katkika kaya maskini Wilaya ya Liwale
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.