Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodlack Mlinga pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakitekeleza agizo lake la kuwaondoa Wakulima na Wafugaji eneo la Hifadhi ya wanyamapori Magingo Liwale (WMA.Wildlife Management Area) agizo hilo alilitoa katika Mikutano ya Vijiji ambapo Kijiji cha Mirui alilitoa tarehe 11/5/2023 na Kijiji cha Kimambi 12/5/2023.
Katika kuwaonda Wakulima na Wafugaji Mheshimiwa Mlinga ameshuhudia makundi makubwa ya ngombe ndani ya hifadhi ya Magingo jambo linalo hatarisha kuhama kwa Wanyamapori na hata uoto wa asili kupotea na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa cha uwaribifu wa mazingira ndani ya hifadhi .
Aidha Mkuu wa Wilaya amejionea baadhi ya wafugaji wakiwa wemeanzisha makazi na kujenga maboma na Mazizi ndani ya hifadhi pia wameanzisha mashamba makubwa kwajili ya shughuli za kilimo na pia wamechimba kisima cha maji ndani ya hifadhi jambo linalo hashiria kuwa shughuli za kibinadamu ni nyingi ndani ya hifadhi.
Pia Mkuu wa Wilaya baada ya ukaguzi wa maboma ya wafugaji ameshuhudia kuwepo na mitego pamoja na pembe ya mnyamapori aina ya Seble (Antelope) ambapo hizo “amezitaja kuwa ni nyara za Serikali ambapo amebaini kuwa licha ya kuwa wafugaji ndani ya hifadhi pia wapo ambao wanajiusisha na shughuli za ujangili kwenye hifadhi”.
Mkuu wa Wilaya mheshimiwa Mlinga ametoa rai kwa wafugaji wote na wakulima kuondoka mara moja katika hifadhi ya Wanyamapori ya Magingo na kwenda kwenye maeneo ambayo yametengwa kwajili ya ufugaji na kilimo katika Wilaya ya Liwale kwani wakiendelea kubaki katika hifadhi sheria itachukua mkondo wake hivyo waondoke kwa hiyari yao.
Kwa upande wa Afisa Wanyamapori Wilaya ya Liwale ndugu Shigela Jilada amesema ni” vema wananchi waliovamia kuondoka na kuyaacha maeneo hayo ili Serikali iweze kupata wawekezaji wawindaji wa kitalii pia amepongeza kwa baadhi ya wafugaji kuitikia wito wa Mkuu wa Wilaya wa kuhama katika maeneo hayo ya hifadhi”.
Nae Afisa Maliasili na Uhifadhi Mazingira Wilaya ya Liwale Damas Mumwi amezitaka jumuiya zote wapake rangi kuzunguka mipaka eneo la jumuiya ili kutenganisha hifadhi na maeneo ya siyo hifadhi, pia kuweka mabango yanayo tambulisha hifadhi, pia kuweka mawe ya mipaka kwenye kona zote za hifadhi, pia awewataka wananchi wa maeneo hayo kutekeleza agizo la mkuu wa wilaya kuondoka ndani ya hifadhi kwa hiyari yao kabla Serikali ijatumia nguvu kuwaondoa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.