Ziara ya Mkuu wa Wilaya Kata ya Kichonda
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodalack Mlinga ametembelea Kata ya Kichonda yenye jumla ya Vijiji vitatu ambavyo ni Mbuli, Nyela, na Kichonda na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Katika ziara iyo Mkuu wa Wilaya alitembelea vijiji vyote ikiambatana na wataalamu kutoka idara tofauti na kufanya mikutano nakusikiliza kero zinazo wakabili wananchi wa maeneo hayo na kuzitolea ufafanuzi kwa wananchi
Miongoni mwa kero zilizo wasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Kata ya Kichonda ni kuwepo na shida ya upatikanaji wa Maji katika Kata ya Kichonda na hivyo kusababisha wananchi kutumia maji ambayo siyo safi na salama na hata ivyo kufuata maji umbali mrefu ambayo yanatumiwa na mifugo pia.
Ubovu wa barabara kutoka Nyela mpaka Mbuli kwenda Liwale wananchi wamemueleza Mkuu wa Wilaya changamoto ya barabara imekuwa ni kero kwao sababu barabara iyo imekuwa ikitumika kusafirisha mazao kutoka shamabani kwenda kwenye maghala na hivyo kumuomba awasaidie ili iweze kupitika katika vipindi vyote ili iweze kurahisisha usafiri.
Wanyama waribifu tembo imekuwa ni changamoto kwa wananchi wa Kata ya Kichonda na hivyo kumuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia pindi wanapo haribu mazao yao kuwasaidia kupata vifuta jasho na pia kuwasaidia kwa kuwatumia askari wa Wanyamapori kuwatoa katika maeneo yao nakuwarudisha kwenye hifadhi.
Pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua kero ya Mawasiliano kwani katika Kata ya Kichonda na Vijiji vyake kumekuwa na changamoto ya kukosekana kwa mawasiliano hivyo wamemuomba mkuu wa wilaya kuhakikisha wanapata minara ya simu ili kurahisisha mawasiliano katika Kata yao na Vijiji vyao.
Kwa upande wa Pembejeo ni miongoni mwa kero ambayo imewasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya kuwa kunabadhi ya watu wameenza kupata Pembejo na wengine awajapata Pembejeo hizo kutokana na kutosomeka kwenye mfumo na hivyo baadhi yao kukosa Pembejeo hizo na ukiangalia kwa sasa ni msimu wa upuliziaji wa Mikorosho ivyo wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasaidia kutatua changamoto iyo.
Aidha katika kutolea majibu ya kero ya maji Meneja wa maji Wilaya ya Liwale ndugu Rumbika Wegoro amesema kuwa” kwa Kata ya Kichonda kumekuwa na tatizo la watu kuaribu na kukata miundombinu ya maji jambo linalopelekea kukosekana kwa maji katika Kata ya Kichonda na hivyo kuwataka wanachi kutunza miundombinu iyo ili iweze kuwasidia kupata maji safi na salama.”.
Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga baada ya kusikiliza kero na kuzitolea ufafanuzi alitoa Maagizo kwa wataalamu na watendaji wote wa Kata ya Kichonda kuwa watu wote wanao haribu miundombinu ya maji kwa kukata mabomba Meneje wa maji kwa kushirikiana na watendaji wengine ni lazima wafanye uchunguzi ili kuwabaini wanao hujumu na kuwachukulia hatua stahiki.
Pia ametoa agizo kwa Maafisa Ugani wote kuhakikisha wanawagawia wakulima wote ambao wamesajiliwa Pembejeo zao kwa wakati na kama kunachangamoto nyingine basi zifanyiwe kazi kwa haraka ili mkulima apate Pembejeo zake kwani pembejeo hizo zinatolewa bure na Serikali.
Mkuu wa Wilaya amegiza kuwa wanachi wote ni lazima wajitolee kwa kwenye miradi ya maendelo ikiwemo Shule ya Sekondari ya Kichonda ambayo ujenzi wake unaanza sasa na pia wanachi wazawa wepewe kazi ambazo azihitaji wataalamu hivyo wawe kipaumbele na si kutoka sehemu nyingine. Pia ametoa agizo kwa Vyombo kuhakikisha wanafuatilia suala la uzwaji wa ardhi kiholele na kudhibiti hali hiyo katika Kata ya Kichonda.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.