Mkuu wa wilaya ya Liwale Mh. Judith Nguli amefanya ziara kwenye Kijiji cha Mbonde kata ya Nangando . Lengo la ziara hiyo ni ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Kijiji hiko, moja ya changamoto zao ni ukosefu wa barabara, meneja wa tarura alitoa ufafanuzi kua wanasubiri wapima ardhi waonyeshe mipaka na wapime, watathmini ili waandae bajeti alafu waiombee fedha na kuchonga barabara.
Mpima Ardhi Bwana Mikidadi Khalfani aliwasihi wananchi kuchangia ili kukamilisha mradi wa urasimishaji. Pia wananchi walilalamika changamoto ya Wanyama pori kuvamia mashamba ya wakulima Mh. Mkuu wa wilaya aliwasihi wananchi kuendelea kulima kwa sababu kituo kikubwa cha askari ya Wanyama pori Kijiji cha Ngumbu hii itasaidia kupunguza uvamizi wa Wanyama.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.