Mkuu wa Wilaya ya Liwale mheshimiwa Goodlack Mlinga amefanya ziara ya siku tatu ndani ya Kata tatu Kata ya Mlembwe, Kata ya Barikiwa, na Kata ya Makata na Vijiji vyake ili kukagua miradi mbalimbali yamaendeleo na kusikiliza kero za wananchi nakuzitolea majibu.
Mkuu wa Wilaya alitembelea Kata ya Mlembwe ambayo inajumuisha Vijiji vya Ndapata Nambinda, na Mlembwe pia Kata ya Barikiwa ikiwa inajumuisha Vijiji vya Barikiwa, Ndunyungu, na Chimbuko,na Kata ya Makata inayo jumuisha Vijiji vya Mpengere, Kigwema na Mkundi na kusikiliza kero mbalimbali ikiwemo Wanyama waharibifu , tembo ambao wamekuwa wakiaribu mazao na kusababisha wanachi kukosa chakula cha uwakika katika vijiji vyao. Hata ivyo changamoto ya Wanyama waharibifu tembo ni karibia wilayaa nzima ya Liwale .
Wananchi wamueleza Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Mlinga changamoto ya wafugaji ambapo wafugaji wamekuwa wengi katika baadhi ya Vijiji jambo linalopelekea kulisha mifugo hiyo kwenye mashamba na hata kuaribu vyanzo vya Maji kwa sababu wafugaji ni watu wa kuhama kutafuta malisho na maji kwa jili ya mifugo .
kukosekana kwa mtandao katika baadhi ya Vijiji na Kata wananchi wamemuleza Mkuu wa Wilaya kuwa kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano kutokana na baadhi ya vijiji kukosa minara ya simu jambo linalopelekea kutopata mawasiliano ya uwakika na pia kuto kutoa taarifa kwa wakati.
Pembejeo kuchelewa kufika nayo imekuwa ni changamoto kwa wananchi kama walivyo mueleza Mkuu wa Wilaya kuwa Pembejeo zimekuwa hazifiki kwa wakati na hivyo kusababisha kutofanya vitu kwa wakati kama wanavyo shauri wataamu wa kilimo na pia mpaka sasa ugawaji wa pembejeo unategema mtandao wa internet lakini vijiji vingine havina huduma ya mtandao jambo linalopelekea Pembejeo kuchelewa.
Wananchi pia wametoa kero yao ya Umeme kwa Mkuu wa Wilaya kuwa Umeme umekuwa ukichelewa kufika katika Vijiji vyao kitu kinachopelekea kupungua kwa shughuli za uzalishaji hivyo wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanapata Umeme katika vijiji vyao.
Pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanapata nyumba za watumishi katika Kata zao na Vijiji ili watumishi waweze kuwaudumia kwa wakati sababu kuna watumishi wengi wanaishi mjini na vituo vya vyaa kazi ni huku vijijini hivyo tunaomba watumishi wajengewe nyumba za kuishi ili tupate huduma kwa wakati.
Kwa upande wa Barabara pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasiliana na wakala wa barabara vijijini TARURA kuhakikisha barabara zote zinazo unganisha Kata kwa Kata na Vijiji kwa vijiji zinakuwa zinafanya kazi kwa vipindi vyote ili wananchi waweze kuuza na kusafirisha mazao na bidhaa zao kwa wakati na pia wananchi kusafiri kwa wakati.
Pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anawasimamia Viongozi wa Kata na vijiji kufanya Mikutano ya vijiji kama vile takwa la kisheria linavyo taka kwa sababu mpaka sasa kuna baadhi ya Vijiji avijafanya mikutano kwa mwaka mmoja hivyo wananchi wanashindwa kujua taarifa za mapato na matumizi na pia taarifa za maendeleo.
Pia kwa upande wa ardhi wananchi wamekuwa na kero kwa kuwepo na migogoro ya mipaka baadhi ya vijiji na vijiji kama vile Kijiji cha Mlembwe na Kijiji cha Barikiwa na hivyo kupelekea kuzorota kwa mahusiano kati ya Kijiji na Kijiji na pia kupoteza mapato ya Vijiji
Wananchi wamemueleza Mkuu wa Wilaya kero ya upande wa Elimu na kuto kuwepo kwa Walimu wakutosha katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari na pia Walimu wa kike kuto kuwepo katika baadhi ya shule na kuwepo na bovu na uchakavu wa madarasa kwa baadhi ya Shule hivyo wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwasidia ili Watoto wapete Elimu iliyo bora. pia kwa upande wa Madarasa mapya yanayo jengwa ya miradi mbalimbali na nguvu za wananchi ikiwemo mapato ya ndani ya vijiji wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anasimamaia baadhi ya wakandarasi ili waweze kuyajenga madarasa hayo kwa wakati na kwa viwango vinavyo takiwa.
Pia wananchi wamueleza Mkuu wa Wilaya kero yao ya kutopata vitambulisho na namba ya NIDA jambao linalo pelekea kukosa huduma za msingi sababu kuna huduma nyingine zinaitaji ujaze namba ya nida au uwe na kitambulisho ili uweze kupata huduma hizo.
Baada ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Gooldlack Mlinga kusikiza kero ametoa Maagizo kwa husika .
Mkuu wa Wilaya ameagiza mkandarasi anayejenga majengo ya madarasa ya Shule ya Msingi Ndapata kuhakikisha anarekebisha kasoro ambazo zimeonekana kwa viwango ambavyo wamekubalina na miongozo kama inavyo taka.
Aidha mkuu wa wilaya ametoa agizo kwa Kijiji cha Nambinda na Amcos zote na maafisa ugani waanze kugawa pembejeo kwa wakulima walio sajiliwa kwa haraka ili wananchi wapate kwani hizo zinatolewa bure na Serikali. Na pia kuweka alama na mipaka kati ya Kijiji cha Nambinda nae neo la hifadhi la Wanyamapori ili wananchi wasiingie kwenye eneo la hifadhi.
Mkuu wa wilaya ametoa agizo kwa Kijiji cha Mlembwe na Barikiwa kumaliza mgogoro wao wa mpaka na pia kuwambia wananchi ukweli wa jambo hili ili kumaliza mgogoro wao kabla ya tarehe 30 July 2023.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa agizo kwa RUWASA kuwa mradi wa Maji wa Kijiji cha Makata ukamilike kwa wakati ili uweze kutoa huduma kwa wananchi .
Kwa upande wa Umeme Mkuu wa Wilaya ametoa agizo kwa Tanesco na REA kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kama mkataba unvyosema kuwa tarehe 30/10/2023 vijiji vyote vilivyopo Wilaya ya Liwale viwe na Umeme. Napia transifoma ya Umeme kwenye Kijiji cha Mpengere ni ndogo hivyo ifungwe kubwa ili wananchi wapate umeme wa uwakika.
Pia ametoa agizo kwa watendaji wote wa Kata na Vijiji kufanya Mikutano kama Sheria inavyo taka wasiofanya ivyo watawajibishwa na sheria.
Pia amewaeleza wananchi kuwa suala la NIDA atalifatilia na kuwapa majibu hivyo wawe wavumilivu kwa sasa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.