Baraza la Madiwani limekutana katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Halmashauri ambapo ajenda kuu ni kuwasilisha taarifa za Kata, mapato na matumizi ya Kata na changamoto pamoja na kujadili miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na kumpitisha mwekezaji katika Kata ya Kichonda ambapo kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo.
Baraza la Waheshimiwa madiwani wamejadili juu ya changamoto ambazo zipo kwenye Kata zao ikiwemo changamoto ya nyumba za watumishi, wanyama waharibifu ambao wamekuwa wakiharibu mazao yao tembo, uvamizi wa mifugo katika maeneo ya wakulima, changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano ya simu na mabweni ya wanafunzi.
Aidha wamepongeza jitihada zinazofanywa na watendaji wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato na kuomba kuongeza nguvu katika kukusanya ili mapato yatumike katika kuleta maendeleo pia wameongeza wakiomba kufanyiwa kazi changamoto zote ambazo zipo ikiwemo kuhakikisha hoja za wakaguzi zinajibiwa na kufutwa pia wameomba Halmashauri kuwasaidia katika miradi ambayo imekwama ili iweze kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi, aidha waheshimiwa madiwani kwa pamoja wamekubali kumpitisha mwekezaji kupewa hekari 1000 katika eneo la Kata ya Kichonda.
Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amewaeleza Waheshimiwa Madiwani na baraza juu ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Liwale ikiwemo kwenye ujenzi wa barabara, madarasa, usambazaji wa umeme vijijini, usimamizi wa maliasili za misitu, na madini pamoja na kusumami upande wa kilimo.
Pia Mheshimiwa Mlinga amewambia Waheshimiwa Madiwani jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na changamoto za uvamizi wa mifugo ambapo Wilaya ya Liwale imetenga eneo la Kata Kimambi na kugawanywa kwa wafugaji na kuyaendeleza maeneo hayo kwa kupanda nyasi na kuchimba visima vya maji katika maeneo yao pia kwenye upande wa wanyama waharibifu tembo Mheshimiwa Mlinga amewaeleza Waheshimiwa Madiwani kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani wameleta mradi wa GIZ ili kutuoa mafunzo na vifaa ili kupambana na wanyama hao waharibifu.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewataka Madiwani kuwa wasimamizi katika Kata zao na kuhakikisha kuwa wanawasimamia watumishi wote katika Kata zao na pia wakae kwenye vituo vyao vya kazi kwani wengi wao wamekuwa hawakai kwenye vituo vyao pia amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia rasilimali za misitu kwenye maeneo yao kwani kumekuwa na uvunaju haramu na kutofuta taratibu na sheria katika uvunaji pia amewakumbusha kusimamia miradi ya maendeleo kwenye Kata zao.
Aidha Mkuu wa Wilaya amegiza Watendaji wa vijiji na Kata kuhakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo katika maeneo yao na pia kusimamia ulinzi na usalama wa Kata na Vijiji kwani kwa sasa ni msimu wa korosho na hivyo matukio yamekuwa mengi sana watu wanaiba korosho kwenye mashamba hivyo amewataka wakawe walinzi kwenye maeno yao.
Picha mbalimbali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.