Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Goodluck Mlinga leo Aprili 22 2024 amezindua rasmi zoezi la utoaji wa Chanjo ya HPV dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale.
Chanjo ya HPV ni chanjo inayotumika kwaajili ya kutoa kinga dhidi ya Virusi vya Human Papiloma HPV vinavyo sababisha Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa kina mama na hivyo kupunguza vifo vitokonavyo na virusi hivyo.
Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa Chanjo hii iliidhinishwa na Shirika la Afya Duniani na nchini Tanzania iliidhinishwa na Wizara ya Afya mwaka 2014 kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA, na pia amepongeza ushirikiano ulipo kati ya Idara ya Elimu na Afya katika kufanikisha zoezi la utoaji wa chanjo hii linafanikiwa vizuri.
Wilaya ya Liwale inalenga kuwafikia na kuwapatia chanjo Wasichana wapatao 7340 kwa lengo la kufikia asilimia 80 kati ya wasichana 9174 katika kipindi cha tarehe 22 hadi 28 April, 2024 ambayo ni wiki ya chanjo Afrika na pia utafanyika ufatiliaji na utoaji wa chanjo zingine kwa watoto wasiopata na wasio kamilisha ratiba ya chanjo.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa Wilaya ya Liwale inafikia kiwango kilicho pangwa na zaidi kwa kujitokeza kwa wingi na kuwaruhusu wasichana wenye umri huo kupata chanjo wakiwa mashuleni na pia Watendaji wa Kata na Vijiji kusaidia kuwatambua walengwa walio nje ya shule na kutoa ushirikiano ili wapatiwe chanjo.
Picha mbalimbali katika zoezi la uzinduzi wa chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi hospitali ya Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.