MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA LIWALE MH. MOHAMMED MTESA AMEKABIDHI PIKIPIKI 35 KWA MAAFISA KILIMO.Mh. Mwenyekiti ameishukuru Serikali kwa kutoa pikipiki kwa Maafisa Kilimo katika Wilaya ya Liwale na amewaasa Maafisa Kilimo kutoa huduma kwa wakulima wote kwasababu Lengo la serikali kutoa pikipiki hizo ni kufikia wakulima wote, ili kuongeza hali ya uzalishaji na mapato kwa ujumla.Pia amewaasa Maafisa kilimo kuhamasisha wakulima kutumi mbolea, kwani Wilaya ya Liwale iko chini kwenye matumizi ya Mbolea.Sambamba na hayo amewataka Maafisa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya viwatilifu katika zao la korosho ili kuongeza ubora wa korosho na kuongeza uzalishaji wa korosho.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.