Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga leo amefunga rasmi mafunzo ya Jeshi la Akiba ambayao yalinza 14 july 2023 yakiwa na wanafunzi 132 ambapo wanawake 33 na wanaume 99 na kumalizika 22 novembar ambapo wahitimu ni jumla ya 85 wanawake wakiwa 19 na wanaume 66 mafunzo hayao yamechukua takribani wiki 18 ambapo wahitimu wamepata mafunzo mbalimbali.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya Meja GC Masinde ambaye ndiye Mshauri na Mkufunzi wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Liwale amesema kuwa sababu za kupungua kwa vijana ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, nidhamu mbaya, kutomudu changamoto mbalimbali za mafunzo
Aidha Meja Masinde amesama kuwa shabaha ya mafunzo haya yamekusudia kumtayarisha kila mwananchi katika utayari na utimamu wa Ulinzi wa Taifa na ni kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taifa namba 24 ya mwaka 1966 pia mafunzo haya yatawapa uwezo askari hawa kufanya kazi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa weledi mkubwa na pia wamepata mafunzo ikiwemo silaha ndogondogo,utimamu wa mwili, vita vya msituni, usomaji wa ramani, kwata mbalimbali, usalama wa taifa, ujanja wa porini na huduma ya kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga katika kufunga mafunzo hayo amewapongeza askari wote walio hitimu mafunzo hayo kwani ni uzalendo mkubwa wameweza kuonesha kwa kipindi chote hicho ambacho wamejifunza na sasa wanarudi kwenye jamii hivyo watatumika kulinda jamii napia wataimarisha ulinzi na usalama wa vijiji vyetu.
Mheshimiwa Mlinga amewetaka askari hao kuhakikisha wanalinda kiapo ambacho wameapa na kuhakikisha wanakuwa watu wema na walinzi wa jamii kwa kusimamia yale ambayo wamejifunza kwa wakati wote wa mafunzo na pia kuhakikisha wanashiriki katika kulinda nakuwa kwenye Kamati za Ulinzi wa Kata na Vijiji katika maeneo yao.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ameongeza kwa kuwataka askari amabo wamehitimu mafunzo hayo ya Jeshi la Akiba kuhusika kwenye kuzuia kungia kwa mifugo ambayo inaingia katika Wilaya yetu na Vijiji vyetu na pia kuacha kutumia mafunzo hayo vibaya kwa kuwaonea wananchi bali wakawe raia wema na kulinda jamii .
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga ametoa maelekezo kwa Taasisi mbalimbali ambazo zipo ndani ya Wilaya ya Liwale kuhakikisha zinatumia walinzi ambao wana mafunzo na kuwataka vijana wambao wamehitimu kupewa kipaumbele katika fursa ambazo zitatokea ikiwemo za ulinzi kwenye kampuni mbalimbali.
Kwa upande mwengine Mheshimiwa Mlinga mamtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuwatumia askari hawa katika kulinda na kukusanya ushuru katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Liwale na pia kutenga bajeti kwa ajili ya kombati na viatu na pia kusiwepo na mtu yeyote kuchangishwa na pia kuhakikisha Taasisi nyingine kuwatumia askari hawa katika mambo mbalimbali.
Picha mbalimbali katika kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.