ZIARA YA UFUATILIAJI WA CHANGAMOTO ZA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE (SCHOOL INFORMATION SYSTEM-SIS) WILAYANI LIWALE.
Wakuu wa Shule za msingi Mbalimbali Wilaya ya Liwale walihudhuria semina ya mafunzo ya mfumo wa taarifa za shule (School Information System-SIS) leo tarehe 03 Juni 2019 yaliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha walimu Liwale (TRC).
Aidha wakati akifungua mafunzo hayo Kaimu Afisa Elimu (Msingi) Mwl. Mussa Shabani aliwaasa Wajumbe kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo wakati wanapotumia mfumo ili wawezeshashaji waweze kutoa majibu na kutatua changamoto hizo.
Mfumo huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia mradi wa Equip-Tanzania na kunufaisha Mikoa Takribani tisa (9) nchini Tanzania ukiwemo Mkoa wa Lindi umekuwa chachu ya kubwa ya kuongeza kiwango cha Ufaulu kwa wanafunzi na Maendeleo katika sekta hii ya Elimu Nchini.
Lakini pia wawezeshaji wa mafunzo Ndg.Erick Makoye (Msimamizi wa (SIS) kutoka makao makuu ya Equip-Tanzania) na Ndg. Kulwa James Masaya (Afisa Taaluma na Mlezi wa SIS Mkoa) walipokea changamoto kutoka kwa wajumbe na kuzitatua changamoto hizo sambamba na kutoa Elimu zaidi juu ya matumizi sahihi na salama ya vishikwambi na Mfumo wa SIS.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.