Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Goodluck Mlinga, amepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha kupatikana kwa dawa ya kudhibiti ugonjwa wa unyaufu fusali, kupitia ushirikiano kati ya TARI Naliendele na Bodi ya Korosho. Amesema hatua hiyo imekuja wakati muafaka, kufuatia kuonekana kwa ugonjwa huo kwenye baadhi ya mashamba ya mikorosho wilayani Liwale.
Akiwasilisha shukrani hizo wakati wa makabidhiano ya dawa hizo, Mhe. Mlinga alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuwalinda wakulima na kulinda uzalishaji wa korosho. Amewahimiza wakulima kuwasiliana na maafisa ugani mara tu wanapoona dalili za ugonjwa ili hatua za kitaalamu zichukuliwe mapema.
Wataalamu kutoka Bodi ya Korosho na TARI Naliendele wamebainisha kuwa takribani hekta 378 tayari zimeathiriwa, na mpango wa kupuliza dawa katika maeneo yote husika unaendelea. Utafiti uliofanywa pia umethibitisha asili ya ugonjwa huo, na hatua za udhibiti zimeanza ili kuzuia kuenea kwake katika maeneo mengine.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele, Dkt. Geradina Mzena, amesema utafiti uliofanywa wilayani Liwale umethibitisha uwepo wa ugonjwa wa unyaufu fusali, na ujio wa wataalamu hao umeelekezwa katika udhibiti na kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.