Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Liwale anawatangazia watendaji wa vituo vya Kupiga Kura waliochaguliwa kwa nafasi za Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji wa Vituo vya Kupigia Kura kuhudhuria mafunzo ya kazi hiyo.
Mafunzo hayo yatafanyika tarehe 25 Oktoba, 2025 kwa Makarani Waongozaji wa Vituo vya Kupigia Kura na 26 – 27 Oktoba, 2025 kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura kuanzia saa 01:00 asubuhi katika vituo vifuatavyo:-
1. Tarafa ya Kibutuka kituo ni Shule ya Sekondari Kibutuka.
2. Tarafa za Liwale Mjini na Makata kituo ni Shule ya Sekondari ya kutwa Liwale (Liwale Day).
Fika ukiwa na Kitambulisho chochote au barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.