Thursday 19th, September 2024
@
Na Michael Ngowi Liwale
Kufatia taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kutangaza kuwepo na mvua za E-linino baadhi ya maeneo ukiwemo baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini Kamati ya Maafa ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imekutana na kujadili ajenda mbalimbali lengo likiwa ni kukabilina na kujianda na mvua hizo katika Wilaya ya Liwale.
Katika kikao hicho kilicho ongozwa na Afisa Utumishi Ndugu kalokola Kasimbazi kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali na wakuu wa taasisi za umma na binafsi wamejadili ajenda mbalimbi ambazo lengo likiwa ni kujiandaa kikamilifu kabla maafa ayajotokea.
Aidha kamati ya Maafa ya Wilaya imekubaliana kupitisha mpango wa utekelezaji wa dharura wa kukabiliana na athari za El-nino sambamba na hilo nikutambua maeneo mbalimbali ambayo yataathirika kama vile mazao, kuharibika, miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kutokea kwa magonjwa ya mlipuko, uharibifu wa mfumo wa majitaka na maji yaliyotuhama na kutiririka katika vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano.
Kwaupande mwingine Kamati imepitia mpango wa utekelezaji na kukubaliana nao na hivyo kuanza kufanyiwa kazi mara moja ikiwemo kutoa taairifa mara kwa mara na pia kuwajulisha wananchi taarifa za mamlaka ya hali ya hewa na tahadhari za kuchukua.
Baadhi ya wajumbe walio shiriki katika kiako kazi chaa maandalizi ya na kuchukua taadhaari za mvua za E- l nino Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.