Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Liwale mkoani Lindi, Bw. Winfrid Tamba, ametangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa ubunge kwa jimbo hilo ambapo jumla ya wapiga kura 56,659 kati ya 93,390 walioandikishwa walijitokeza kupiga kura. Kati ya kura zilizopigwa, kura halali zilikuwa 56,436 huku kura 223 zikitajwa kuwa batili.
Akitangaza matokeo hayo, Bw. Tamba amesema kuwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Munde Mshamu Ali, ameibuka mshindi baada ya kupata kura 52,552, sawa na asilimia 93.1 ya kura halali. Aliyefuata ni mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaibu Saidi, aliyepata kura 1,776 (3.1%), akifuatiwa na Maude Hassan Jabir wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 1,751 (3%). Mgombea wa CHAUMA, Mikidadi Abdala, alipata kura 357, sawa na asilimia 0.6.
Kutokana na ushindi huo, Bw. Tamba amemtangaza rasmi Munde Mshamu Ali wa CCM kuwa Mbunge mteule wa Jimbo la Liwale na kumkabidhi cheti cha ushindi. Shughuli hiyo imefanyika kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, na imehitimisha mchakato wa kumpata mwakilishi wa wananchi wa Liwale katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.