Baraza la Madiwani la Pitia Taarifa ya Utendaji na Uwajibikaji
Baraza la Madiwani limekutana leo katika mkutano wa kawaida wa mwaka na kujadili ajenda mbalimbali katika mkutano huo ambao ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara na Vitengo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Liwale day.
Katika mkutano huo wajumbe walipitia taarifa ya utendaji na uwajibikaji ya mwaka 2022-2023 kwa idara mbalimbali na kujiridhisha na kutoa mapendekezo sehemu zenye changamoto ziweze kufanyiwa kazi ikiwemo kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri na pia kutatua changamoto zinazo wakabili wananchi.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameshauri Elimu itolewe kwa watendaji juu ya matumizi ya mifumo ya fedha ili watendaji waelewe na” pia wameomba mifumo ya fedha iboreshwe kwa kuondoa ukomo kwenye matumizi kwani vijiji vingi vinakusanya mapato mengi ila kwenye matumizi ya makusanyo hayo yamekuwa na ukomo hivyo mifumo ikirekebishwa tutaweza kutumia fedha hizo katika miradi ya maendeleo kwa wakati”.
Pia Madiwani wamemeshauri na kupendekeza kuwepo na mikakati juu ya kutoa Elimu ya ukatili wa Kijinsia ili ili wananchi wapate uwelewa juu ya ukatili aidha Diwani wa Kata ya Likongowele Msheshimiwa Mkoyage ameshauri kuwepo na ujenzi wa vibanda eneo la Zain ili kuiyongezea mapato ya kudumu Halmashauri ambayo itasaidia kukuza maendeleo na mapato kukua.
Aidha Baraza lilimchagua na kumpitisha Mheshimiwa Mohamed Likoko Diwani wa Kata ya Liwale mjini kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na pia baraza lilichagua Kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya kudhibiti Ukimwi, kamati ya Maadili, kamati ya Elimu Afya na Maji na kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.