Baraza la Madiwani limepitisha bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale jumla ya shilingili bilioni 26,779,558,036.00 kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025 ikiwa ni ruzuku kutoka Serikali Kuu, mapato ya ndani fedha za wahisani na matumizi mengineyo, mishahara na miradi ya maendeleo.
Bajeti hiyo ambayo itakwenda kutekeleza miradi ya maendeleo na mambo muhimu ambayo yamezingatiwa ikiwemo kumalizia miradi viporo kwa majengo ya kutolea huduma kama vile Shule na Zahanati, kutenga fedha kwaajili ya watu wenye mahitaji maalumu, kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwaa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyo sajiliwa vya Wanawake na Vijana na watu wenye Ulemavu pamoja na kugharamia miradi ya maendeleo na kutenga fedha kwaajili ya kuimarisha shughuli za Kilimo.
Hata hivyo maoni ya Waheshimiwa Madiwani yaliyo tolewa kwenye kamati za kudumu ya meonyesha muelekeo chanya katika maandalizi ya mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/ 2025 ikiwemo Baraza la Wafanyakazi, Kamati ya Ukimwi, Kamati ya Elimu Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango.
Aidha katika Baraza hilo la kupitisha bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Goodluck Mlinga amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote kwa kuwa wafatiliaji wa miradi ya maendeleo na mambo mengine ya msingi katika Kata zao na kuwataka waendelee kuwasaidia na kutatua changamoto za wananchi wao.
Katika Baraza hilo Mheshimiwa Mlinga amewakumbusha Madiwani wote kuhakikisha wanafatilia na kuchukua hatua kwa kushirikiana na viongozi wa Vijiji na Kata kwa wanafunzi ambao bado hawajaripoti kwenye shule ambazo wamepangiwa mpaka sasa uripoti wa wanafunzi wa kidato cha kwanza hauridhishi hata kidogo hivyo tunawajibu wakulisimamia hili na pia kwa wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shule nao watachukuliwa hatua.
Pia Mheshimiwa Mlinga amewataka Madiwani kwa sasa kuendele kuwakumbusha wananchi kuwa mvua zinazoendelea kunyesha ni nyingi hivyo sio vyema kuendelea kulima mabondeni badala yake walime katika maeneo ambayo ni sahihi ambayo siyo hatarishi na pia waendelee kuchukua taadhari kwani mpaka sasa bado mvua zinaendelea kunyesha na pia napenda kutoa wito kwa wananchi wote tulime mazao ya chakula ili kuongeza upatikanaji wa chakula kwa wingi na tuache kulima mazao yale ya maozoea na barabara zetu pia zimekuwa na changamoto ila zinafanyiwa kazi na zitaendelea kupitika.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mlinga amewambia Madiwani kuwa changamoto nyinginezinaendelea kufanyiwa kazi kama vile Serikali ilivyo haidi ikiwemo changamoto ya mifugo wote tumeona Taskforce ambayo ilikuwepo hapa na kuzunguka kote na kutoa elimu kwa wafugaji katika maeneo yao na hivyo kila mfugaji atapewa eneo lake na kulihudumia kwa kupanda nyasi na kuchimba visima pia amewataka Madiwani kwenda kusimamia Kamti zao ardhi za Vijiji na Kata ili kudhibiti uuzwaji ardhi wa holela kwenye Vijiji na kuhusu wanyama waharibifu bado Serikali inafanyia kazi na matokeo tumeyaona hivyo tuendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali yetu ili tuweze kutekeleza haya yote .
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amewataka na kuwakumbusha Madiwani wa Kata zote kuwa wasimamizi wa mali zao ikiwemo kusimamia Kamati za Maliasili za Vijiji katika uvunaji wa misitu huko tumeona mambo ambayo yanafanyika na pia tukasimamie uvamizi wa watu ambao wanakuja kuchimba madini na kuyatorosha kwani tusipo simamia tutapoteza mapato ya Halmashauri na Vijiji.
Baadhi ya wajumbe mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Madiwani, pamoja na Wakuu wa Idara ambao wamehudhuria katika Baraza la kupitisha Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika ukumbi wa shule ya Liwale Day.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.