Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amezindua mafunzo ya Jeshi la Akiba katika Kata ya Kibutuka Kijiji cha Kibutuka ambapo jumla ya wanafunzi 60 wamejiandikisha katika mafunzo hayo ambayo yanatarijiwa kuchukuwa wiki 18 mpaka kuhitimishwa kwake.
Katika ufunguzi huo Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa atahakikisha wanafunzi wote watapata sare zote ambazo zimeombwa na mkufunzi wa mafunzo hayo Meja Gamwaka Masinde napia aimeitaka Halmashauri kuhakikisha wanachangia gharama ambazo zimetajwa ili kuwapa hari vijana kushiriki mafunzo hayo.
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amevitaka Vijiji vyote ambavyo vina mapato washiriki wake wanaoshiriki mafunzo hayo kuhakikisha wanachangia gharama za sare pamoja na mahitaji mengine ili kuhakikisha mafunzo haya yanaendeshwa kwa ustadi mkubwa na kuondoa changamoto ambazo zinaweza kujitokeza.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ametoa rai kwa wanafunzi ambao wanashiriki mafunzo hayo ya jeshi la akiba amewataka washirikiane na viongozi wa Vijiji na Kata kuhakikisha wanashirikiana na wakufunzi wa mafunzo hayo kuwasaidia vijana hao ili waweze kuhitimu mafunzo hayo ambayo yanaendelea katika Kijiji cha Kibutuka.
Kwa upande mwengine Diwani wa Kata ya Kibutuka Mheshimiwa Faraji Mnyihira amesema kuwa “anafuraha kubwa kwa mafunzo hayo kufanyika katika Kata ya Kibutuka kwani yatasidia vijana kupata mafunzo na kushiriki katika oparasheni mbalimbali ikiwemo kuondoa mifugo na pia kulinda amani katika vijiji mbalimbali na kushiriki katika shughuli za uchaguzi katika Wilaya ya Liwale hivyo amehaidi kutoa ushirikiano wakutosha ili kuhakikisha mafunzo hayo yanafanikiwa”.
Picha mbalimbali katika ufunguzi wa mafunzo wa Jeshi la Akiba katika kijiji cha Kibutuka Kata ya Kibutuka
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.