Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefanya ziara ya kutembelea migodi ya madini katika eneo la Kata ya Kibutuka kitongoji cha Kiomanilo, Kata ya Kiangara Kijiji cha Litou na Kata ya Mangirikiti Kijiji cha Ngorongopa.
Mheshimiwa Mlinga ametembelea nakujionea shughuli za uchimbaji wa madini mbalimbali ikiwemo Manganize, Beliriamu, Dhabu, Mabo, na madini ya Safaya ambapo Mheshumiwa Mlinga amesisitiza kuhakikisha Halmashuri inafatilia na kujua shughuli zote zinazofanyika ili iweze kukusanya mapato ambayo yanatokana na madini hayo.
Hata hivyo Mweshimiwa Mlinga ameitaka Halmashauri kufuatilia migodi yote na wamiliki wote wa leseni ambao wapo ndani ya Wilaya kujua Halmashauri inakusanya kiasi gani kutoka kwenye migodi hiyo, na pia kudhibiti wimbi la utoroshwaji wa madini ambayo yanaenda kuunzwa sehemu nyingine na kusababisha Halmashauri kupoteza mapato, na pia amewataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanafatilia mizigo ina yotoka katika migodi ili kuweza kupata uhalisia wa mizigo inayo toka kwenye migodi ambayao itasadia kutupa dira ya kukusanya mapato ya Halmashauri kwa uwakikia.
Mheshimiwa Mlinga amewataka viongozi wote wa vijiji kuhakikisha wanawasimamia na kuwafatilia wachimbaji wote ambao ni wakubwa yaani wawekezaji katika maeneo yao wanapata stahiki za vijiji na pia kufatilia ahadi ambazo walihaidi kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji wengi wa wawekezaji wamekuwa wakitoa ahadi lakini azitekelezeki hivyo tufatilie na pia viongozi wa vijiji tuisaidie Halmashauri iweze kukusanya mapato kwa kutoa taarifa sahihi.
Aidha Mweshimiwa Mlinga ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wadogo kuhakikisha wanajisajili na kuwa na viongozi na vikundi ambavyo vinatambulika ili waweze kupata leseni zao na pia itasaidia kuepuka usumbufu wa kufukuzwa katika maeneo yao na wachimbaji wakubwa na pia kuwatambua watu ambao wanajishughulisha na uchimbaji na waalifu kumekuwa na watu wanafanya uhalifu na kukimbilia kujificha kwenye migodi hivyo tunawajibu wa kujuana ili tuweze kufanya kazi zetu kwa amani na utulivu.
Pia Mweshimiwa Mlinga amewataka wachimbaji wote wanapoenda kuuza madini katika Wilaya jirani wa hakikishe kuwa wanasema ni wapi wanachimba madini hayo kwani Wilaya ya Liwale imekuwa na wachimbaji wengi na madini mengi ya aina mbalimbali likini Halmashauri haipati ushuru wake kutokana na wachimbaji kutokutoa a taarifa za ukweli hivyo nilazima tusema kuwa madini haya yanatoka Liwale ili tuweze kupata ushuru wetu.
Picha mbalimbili katika ziara ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Goodluck Mlinga na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kutembelea migodi mbalimbali .
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.