Katibu tawala Wilaya Bi Azilongwa mwinyimvua Bohari leo tarehe 29/7/2025 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC).
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Liwale day na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini, vyama vya siasa, Wakuu wa taasisi za umma na binafsi pamoja na watendaji wa serikali kutoka katika ngazi mbalimbali.
Lengo la kikao hicho ni kujadili na kutoa maoni/mapendekezo kuhusu mpango wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025-2050 ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kupata ushiriki mpana wa wananchi kutoa maoni yao.
ili kuhakikisha hakuna mtu au kundi linaloachwa katika mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya 2025-2050 kama ambavyo alielekeza Mhe Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mapendekezo/maoni ambayo wadau/ washiriki wametoa katika kikao hicho kuelekea maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yamejikita zaidi katika masuala yanayohusu biashara na uwekezaji, kilimo, elimu, afya, uhifadhi wa misitu na mazingira, utalii, matumizi sahihi ya rasilimali, ajira, upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa viwanda, Suala la malezi na maadili pamoja na matumizi sahihi ya teknolojia.
Mpango wa ushirikishaji wadau/wananchi katika zoezi la ukusanyaji wa maoni kuelekea maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ulizinduliwa na Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 9/12/2023 katika kikao cha kwanza cha taifa cha Dira 2050 ya Maendeleo ya Taifa.
Picha mbalimbali katika Kiako cha DCC ambapo makundi mbalimbali yametoa maoni yao juu ya Dira mpya ya Taifa Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.