Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale wamefanya ziara ya kwenda kujifunza biashara ya hewa ukaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi lengo ikiwa ni kuachana na biashara ya uvunaji wa magogo na kuingia katika biashara hiyo ili kuweza kukuza mapato ya Halmashauri.
Katika ziara hiyo hili hudhuriwa na Waheshimiwa Madiwni, Mkuu wa Idara ya Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Ndugu Deogratias Justus Simwanza, pamoja na Maafisa wengine ambao waliambatana hata hivyo madiwani wamewaza kupata elimu juu ya ufadhi wa misitu ya asili ambayo ndio uti wa mgongo katika biashara hiyo ya hewa ya ukaa na pia walijifunza namna biashara hiyo itakavyo ongeza mapato kwa Halmashauri na vijiji vitakavyo nufaika na miradi ya maendeleo kupitia biashara hiyo ya hewa ya ukaa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Mohamed Mtesa “amesema kuwa wao kama Madiwani wanakazi kubwa ya kwenda kuifanya kwa wananchi wao kwa kuwapa elimu ambayo itawasaidia kuondoka kwenye biashara ya kuvuna magogo na kuanza kuhifadhi misitu ili vijiji viweze kuingia kwenye biashara hii ya hewa ya ukaa.
Tumeona wenzetu wa Halmashauri ya Tanganyika jinsi wanavyo pata mapato makubwa kiasi cha shilingi bilioni 17 kwa mwaka kutokana na kuhifadhi misitu kwa maana hiyo hata sisi Halmashauri ya Wilaya ya Liwale tunaweza kuhifadhi nakuingia kwenye biashara hii ambayo itakwenda kunufaisha Halmashauri na vijiji kwa kupata miradi ya maenendeleo ikiwemo madarasa, vituo vya afya na zahanati, nyumba za wahudumu wa afya na walimu pamoja na viongozi wa vijiji katika maeneo husika.
Pia Halmashauri ina nafasi kubwa ya kuwatumia wataalamu wake kuhakikisha wanasaidiana na madiwani kwa kuwapa elimu wananchi wetu juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu na pia kuanza kudhibiti uvunaji wa magogo ambao unafanyika katika vijiji vyetu kwa sababu biashara hii inahitaji tutunze misitu.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kwasasa ina kazi ya kuhakikisha kuwa misitu yote inayo milikiwa na Halmshauri ina pata utambuzi wa majira nukta na pia kutangaza katika gazeti la Serikali ili Halmashauri iweze kumiliki misitu yake kisheria na iweze kuingia kwenye biashara hiyo ya hewa ukaa.
Hata hivyo Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale wameshahuriwa kuhakikisha wanaelewa biashara hii ya hewa ya ukaa kwa undani zaidi kabla ya kuingia na pia kuelewa changamoto ya biashara hiyo na kuweka mikakati madhubuti ya usimamizi kabla ya kungia mikataba na wanunuzi wa hewa ya ukaa.
Waheshimiwa Madiwani wakifatilia mafunzo ya biashara ya hewa ya ukaa kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Picha mbalimbali za ziara ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi katika kujifunza biashara ya hewa ya ukaa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.