Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Goodluck Mlinga, amekutana na wazazi pamoja na wanafunzi 37 wa shule ya sekondari Hangai, Kata ya Ngongowele katika juhudi za kuhamasisha elimu miongoni mwa watoto pamoja na ushirikiano kati ya wazazi na viongozi ili kuhakikisha watoto wanapata elimu stahiki na kuacha utoro.
Mhe. Mlinga amesisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto, akisema, "Chini ya miaka 18, mtoto anapaswa kwenda shule kupata elimu." Ameonya kuhusu athari za kutohudhuria shuleni, akieleza kuwa watoto wanaokosa masomo wanakumbana na hatari ya kukosa fursa za maisha bora.
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wazazi kuandika barua ya kuahidi kusimamia watoto wao wahudhurie shule amesema ushirikiano wa wazazi na viongozi ni muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata elimu, kwani elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Mlinga amesisitiza wajibu wa wazazi katika kuwalazimisha watoto wao kusoma. "Tujitahidi kuwalazimisha watoto wetu kuhusu umuhimu wa elimu ili kuongeza idadi ya wanafunzi walioelimika," amesema.
Aidha Mhe. Mlinga ameahidi kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wazazi au walezi watakaoshindwa kutimiza makubaliano hayo, Ameeleza kuwa ni muhimu kwa jamii kushirikiana ili kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya misingi ya elimu.
pia Mkuu wa Wilaya ametoa rai kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha watoto wanapata elimu. "Sote tumepewa jukumu la kuwasaidia watoto wetu kufikia malengo yao ya kielimu,” hivyo tuna wajibu wa kusimamia watoto wetu kuhakikisha wanapata elimu na kuthibiti utoro mashuleni.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale katika matukio ya wazazi na wanafunzi ambao ni watoro mashuleni.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.