Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimwa Goodluck Mlinga ametaeu Baraza la Michezo la Wilaya ya Liwale ambalo linashirikisha michezo mbalimbali lengo likuwa ni kuibua vipaji na kuviendeleza na pia kujenga afya kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.
Katika utambulisho huo ambao ulitanguliwa na bonanza la michezo lililofanyika katika viwanja vya michezo vya Wilaya ya Liwale ikiwemo michezo mbalimbali ambayo washiriki walishiriki jogging, mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, karate, boxing, ngoma za asili, mechi ya Wakuu wa Idara na Madiwani pamoja na mechi maalumu kati ya Mashabiki wa Simba na Yanga.
Katika michezo hiyo Wakuu wa Idara waliibuka washindi wa bao 2 kwa 1 dhidi ya madiwani na wakuu wa idara wameibuka na zawadi ya mbuzi mmoja na mechi ya mashabiki wa wa yanga waliibuka na na ushindi wa penati 6 kwa 5 na kujishindia ngombe mmoja na pia washiriki wengine walijishindia mechi na kujipatia zawadi mbalimbali.
Katika bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Mlinga amewataka washiriki wa michezo mbalimbali kuhakikisha wanashiriki michezo hiyo kwani michezo ni afya na michezo inaleta amani na inajenga ushirikiano hivyo watumishi pamoja na wananchi tushiriki katika michezo ili tuborshe afya zetu
Na pia Mheshimiwa Mlinga amewahidi wanamichezo wote walio shiriki michezo mbalimbali kuwa changamoto zote ambazo walizo nazo Serikali inatambua na “niwahidi kuwa Serikali hii ya sasa inatambua uwepo wa michezo na inatambua kuwa michezo ni ajira hivyo changamoto zitafanyiwa kazi ili michezo iweze kusonga mbele.
Hata hivyo pia amewapongeza washindi mbalimbali walioshinda katika bonanza hili lamichezo ikiwemo wataalamu kutoka Halmashauri, kwa kuwashinda Madiwani na pia mashabikiwa wa timu ya yanga kwa kuibuka na ushindi dhidi ya mashabiki wa timu ya simba na kushinda zawadi ya ngombe mmoja hivyo tutumie michezo kutuunganisha na kutujenga.
Washiriki wa michezo wakishiriki michezo mbalimbali Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.