Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amemtengua Mwenyekiti wa kijiji cha Kipelele Ndugu abruhaman Abdallah Mnoile kwa tuhuma za kuongoza uzwaji wa ardhi kiholelea bila kuchukua hatua yoyote kwa wahusika jambo linalopelekea kuibuka kwa migogoro ya ardhi katika kijiji hicho aidha Mheshimiwa Mlinga Ameteuwa Bi Salma Haji kuwa mwenyekiti wa Kijiji cha Kipelele.
Hayo yamejiri katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga baada ya wananchi kukerwa na mwenendo huo wakuuza ardhi bila kufuta utaratibu ambao upo hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amevitaka vyombo vinavyo husika ikiwemo Polisi na Takukuru kuchunguza walio husika katika kuuza maeneo hayo na wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kuwapeleka Mahakamani na pia amewataka viongozi wa kijiji cha Kipelele na Ngumbu kumaliza kero zao za mipaka kabla ya January mosi
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuisimamia Serikali ya kijiji ili kuweza kudthibiti mambo kama haya yasitokee kwani kuuza ardhi bila kufuta utaratibu ni kosa na hivyo “wale wote ambao pia wamenunua maeneo hapa Kipelele bila kufuta utaratibu wametapeliwa hivyo watoe ushirikiano kwa serikali na vyombo ili tuwabaini wahusika mrudishiwe pesa zenu hayo ameyasema Mheshimiwa Mlinga”.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewakumbusha wafugaji ambao wapo na wamenunua maeneo katika kijiji cha Kipelele kuwa eneo hilo sio kwa ajili ya mifugo bali ni kwajili ya shughuli nyingine hivyo ni bora wakaondaka haraka ili kuepusha matatizo watakayo yapata kwani wafugaji wamekuwa wakilisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na hivyo kuwataka warudi kwenye maeneo yao sambamba na hilo pia Mheshimiwa Mlinga amewaeleza wananchi wa Kipelele kuwa Serikali bado inafanyia kazi kuwepo kwa wanyama waharibifu ikiwemo kutoa mafunzo na pia kuna mradi mpya wa GIZ kutoka Serikali ya Ujerumani ambapo watotaoa mafunzo kwa vijiji ili tuweze kukabilina na wanyama hao .
Pia Mheshimiwa Mlinga amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha anasimamia na kumalizika kwa Wakati kituo cha afya cha Naujombo kilichopo Kata ya Mirui ili wananchi waweze kupata huduma za kitabibu katika maeneo yao na pia amewakumbusha watumuishi wa umma kukumbuka wajibu wao wakutoa huduma kwa wananchi kwa wakati na kuondoa changamoto kwa wananchi na pia watumishi wote wakae maeneo yao ya kazi ni marufuku kwenda kudhurula mjini bila kibali mbaki vituoni mtoe huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akikagua kituo cha afya cha Naujombo Kata ya Mirui.
Muonekano wa kituo cha afya cha Naujombo
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.