Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo amefanya Mkutano na wananchi wa Kata ya Mpigamiti ambaayo ina Vijiji vya Mitawa, Makororo na Mpigamiti ikiwa ni kuwasikiliza na kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
Akijibu hoja ambazo zimetolea na wananchi wa Kata ya Mpigamiti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amewataka Watendaji wa vijiji kuhakikisha wanafanya mikutano yote katika Vijiji vyao na Kata na pia kuwasomea wananchi mapato na matumizi katika mikutano hiyo pia ameongeza kuhakikisha wanakusanya mapato yatokanayo na mazao ili vijiji viweze kupata mapato na Mtendaji ambaye hatafanya mikutano atachukuliwa hatua kwa kuto wajibika sababu serikali inawalipa hivyo mnawajibu wa kuwatumikia wananchi.
Aidha Mkurugenzi amelekeza na kutoa elimu kwa wananchi utaratibu wa kijiji kutoa fedha benki na pia amemuagiza Mkaguzi wa Ndani kuja kufanya ukaguzi katika Kijiji cha Mitawa baada ya wananchi kutoa malalamiko juu ya matumizi ya fedha za kijiji na kutosomewa mapato na matumizi katika mikutano.
Hata hivyo Mkurugenzi amewakumbusha wakazi wa Mpigamiti juu ya kuendelea kuanzisha miradi katika Kata yao na Vijiji vyao ikiwemo ujenzi wa Shule, Zahanati,na kuchangisha na kuanzisha maboma baada ya hapo Serikali italeta fedha na kumalizia hivyo tushirikiane ili tuweze kusonga mbele na kuleta maendeleo katika Kata hii ya Mpigamiti.
Pia Mkurugenzi amewataka wataalamu wakilimo katika Kata ya Mpigamiti kuhakikisha wanafika katika mashamba ya wananchi ambao mazao yao yameharibiwa na wanyamapori iliwawezekurekodi na kuchukua taarifa kwaajili ya kupeleka kwenye Wizara ili wawezekupewa kifuta jasho kutokana na uharibifu uliofanywa.
Hata hivyo Mkurugenzi ametoa wito kwa wazazi kuwajibika kwa kuwasimamia watoto wao kuhudhuria shuleni na kuacha utoro na pia amewewataka kuwapeleka watoto shule hata kama awana sare za shule na pia amewasisitiza katika kuchangia chakula cha shule ili watoto wahudhurie shule na hii itapunguza utoro na pia watoto watapata elimu.
Picha mbalimbali katika Mkutano wa Wananchi na Mkurugenzi Mtendaji Tina Sekambo katika Kata ya Mpigamiti.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.