MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA LIWALE MH. MOHAMMED MTESA AMESHIRIKI KATIKA ZOEZI LA UGAWAJI WA BIMA ZA AFYA YA ICHF ILIYOIMARISHWA KWA WANAFUNZI 18 WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
MH. Mohammed Mtesa amewapongeza Taasisi ya Brighita foundation kwa kusimamia zoezi hilo na kushirikisha wadau kusaidia wanafunzi hao kupata bima hizo. Kadhalika na ustawi jamii kutambua wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Aidha Mh. Mohammed Mtesa amechangia kadi 18 za bima ya afya kwa awamu nyingine ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaoishi kwenye mazingira magumu wanafikiwa na wanapata huduma za afya bila changamoto yoyote.
Mkurugenzi wa taasisi ya Brighita foundation, Brighta Kambona amemshukuru Mwenyekiti wa halmashauri Mh. Mohammed Mtesa kuwepo kwenye uzinduzi huo na kuwachangia wanafunzi kwa awamu nyingine.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.