Wadau na makundi mbalimbali wamekutana katika kujadili changamoto na mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ukatili wanawake na watoto katika wilaya ya liwale ambapo kikao hicho kimeendeshwa na mwanasheria wa Halmashauri ndugu Elibariki Sindato.
Katika kikao hicho kimehudhuria na wadau, makundi mbalimbali, viongozi wa Dini, asasi za kirai, Wanafunzi na jeshi la polisi ambapo mwenyekiti amesema ‘dhumuni la kuitisha kamati hiii ni kuweza kujadiliana juu ya ulinzi wa maisha ya watu hususa ni wanawake na watoto”
Mwenyekiti amewasisitiza wajumbe kwa nafasi zao katika jamii inabidii waweze kuweka mipango na mikakati ya ulinzi wa Wanawake na Watoto ambapo kulingana na takwimu iliyowasilisha na Afisa ustawi wa jamii Bi Ziada Mkungu juu ya matukio ya ukatilii yaliyoripotiwa ofisi ya ustawi wa jamii ambayo imeeonyesha kuwa na idadi ya wahanga 337 walioripotiwa kupatwa na changamoto hizo
Aidha baadhi ya wajumbe walizungumzia swala la wanafunzi wanaojifelisha mitihani yao ya taifa kwasababu ya kutishiwa na wazazi wao, Kaimu afisa elimu msingi Bi. Mwanahiba Mwichande amesema" Wanafunzi ambao wamefeli mitihani ya taifa wanaweza kurudia tena masomo ndani ya miaka miwili". Hiyo itawasaidia wale waliokosa kufanya mitahini kupata fursa kurudia mitihani yao.
Pia kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wanaofanya biashara ndogondogo mitaani kulingana na tabia hii kuwa chanzo Cha kukosa elimu kwa watoto hao, wajumbe wamesisitiza barua ziandikiwe kwa watendaji Kata na Vijiji kuwaita wazazi na waajiri wanaowatuma kazi hizo kuwaita ili kukemea vitendo hivyo na kuwachukulia hatua.
Kwa upande mwingine wajumbe wa kikao wametoa maoni kwa serikali kuhakikisha kunajengwa nyumba maalumu kwa ajili ya wahanga pia kuhamasisha wazazi kuacha kuwalazimisha watoto kujifelisha mitihani yao hivyo maafisa wa jamii ngazi ya Kata, na Vijiji kutoa elimu kwa Wanafunzi na wazazi kuacha tabia hizo.
.
Picha mbalimbali katika kikao cha kupinga ukatili wa kijinsia kilicho fanyika wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.