Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka viongozi na wananchi kutumia takwimu za sensa kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo yao ili kuboresha maisha na ustawi wa watu kiuchumi ameyasema hayo katika uzinduzi wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa kwa viongozi na makundi mbalimbali kutoka Wilaya za Ruangwa Nachingwea na Liwale.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka wiongozi na wananchi kuona umuhimu kutumia matokeo ya sensa katika kupanga mipango ya maendeleo na kuonyesha fursa za uwekezaji ambazo zinapatika katika Wilaya hizi na Mkoa huu matokeo haya yatasaidia kukuza wilaya zetu katika sekta ya uchumi hivyo viongozi tutumie matokeo haya kutangaza Wilaya zetu ili tupate wawekezaji.
Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza umuhimu wa viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata mpka Vitongoji kuwa na taarifa hizi hata pale Kiongozi wa Wilaya atakapo tembela aweanazijua na pia kuwepo na vikao ambavyo vitajadili matokeo haya ili wananchi wawezekujengewa uelewa na waweze kushauri na kutoa maoni na mapendekezo yao juu ya mipango ya maendeleo ya maeneo yao.
Hata hivyo Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Halmashauri wafanye kazi za ya kuuhisha anwani za makazi na kuweka mikakati ya kutunza miundombinu yake kuwa endelevu kwa ajili ya kurahisisha ufikiwaji wa wananchi na kurahisisha biashara mtandao pia amesisitiza na ametaka ufanyike uhakiki wa vibao vilivyo wekwa na pia kuwaelimisha wananchi umuhimu wa anwani hizo wasivingoe kwa sababu vinasaidia kuelekeza mtu anapo kwenda.
Kwa upande mwingine Wilaya ya Liwale ina jumla ya wakazi wapatao 136, 505 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi hivyo matokeo haya yataiwezesha Halmshauri kufanya maamuzi yote ya kibajeti na kupanga miradi ya maendeleo na kufatilia utekelezaji wa mipango ya kisekta ambayo yatasaidia Wilaya kukua kiuchumu na kuongeza ustawi na kubadili maisha ya watu.
Aidha Mheshimiwa Majaliwa amesisitaza kuwa matumizi ya matokeo haya yawe ni ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya kikanuni katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri huku akiwataka viongozi na watendaji wakae pamoja na kupanga mipango bora ambayo itatumika kubadili hali za wananchi na kupanga mipango ya maendeleo katika Wilaya husika.
Picha mbalimbali katika uzinduzi wa mafunzo na usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa kwa viongozi na makundi mbalimbali .
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.